You are currently viewing DIANA B AIREJESHA CHANELI YAKE YA YOUTUBE BAADA YA KUFUTWA NA WADUKUZI

DIANA B AIREJESHA CHANELI YAKE YA YOUTUBE BAADA YA KUFUTWA NA WADUKUZI

Mwana mitandao aliyegeukia muziki Diana Marua amefanikiwa kurejesha akaunti ya Youtube ambayo ilikuwa imedukuliwa mapema wiki hii.

Kupitia ukurasa wa instagram Diana Marua ameshindwa kuficha furaha yake kwa kuipongeza kampuni ya ngoma na uongozi wa Youtube kwa kumsaidia kuirejesha chaneli yake ya youtube yenye subscribers laki 5.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Diana Marua ambapo wameenda na kumshambulia hitmaker huyo wa “One Day” aache suala la kutengeneza kiki mwenyewe kwani aliifuta akaunti yake ya youtube kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa nchini kabla ya ujio wa wimbo wake mpya.

Utakumbuka juzi kati mumewe Bahati alitangaza kuwa Diana B ataachia wimbo wake mpya januari 25 mwaka huu lakini baada ya wadukuzi kuifuta chaneli ya youtube ya mrembo huyo ilibidi mchakato wa kuachia ngoma hiyo iahirishwe.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke