You are currently viewing DIANA B AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA MKE WA MR. SEED

DIANA B AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA MKE WA MR. SEED

Mwana mitandao aliyegeukia muziki Diana B amekanusha kuwa kwenye bifu na mke wa msanii mwenzake mr. Seed.

Akizungumza kwenye ambayo alipewa ubalozi ya hospitali moja jijini Naoirobi, Diana b amekiri kutokuwa na maelewano mazuri na nimo kipindi cha nyuma kwa kusema kwamba hakuwa amekomaa kiakili kushughulikia ugomvi wao kiustaarabu.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mubaba” ameongeza kuwa yeye na Nimo walikuwa hawajakutana kwa muda mrefu lakini kwa sasa wana maelewano mazuri baada ya kuweka kando tofauti zao

“Tofauti zilikuwepo lakini unajua watu hufanya makosa katika miaka yao nyuma na wakati mwingine unagundua labda haujakomaa kiaki kushughulikia maswala fulani kwa njia bora lakini maisha hutufundisha somo,” alisema.

Diana na Nimo waliingia kwenye ugomvi mwaka wa 2018 wakati wa sherehe za Mwaka Mpya ambapo Diana alidaiwa kumdhulumu Nimo vibaya licha ya kuwa mjamzito kipindi hicho.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke