Mwanamitandao aliyegeukia muziki nchini Diana B amefurahishwa sana na kitendo alichofanyiwa na shabiki yake ya kujichora Tatoo yenye uso wake mgongoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diana B ameshindwa kuficha furaha yake kwa shabiki huyo ambapo amewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii wamsaidie kumtafuta mrembo huyo ili aweze kukutana nae kwani amekoshwa na upendo ambao amemuonyesha kwa kuchora tattoo ya uso wake.
Kauli ya Diana B imekuja mara baada ya binti mmoja ambaye ni shabiki yake kuchora tattoo ya uso wa msanii huyo kama njia ya kumuonyesha upendo kwani anazikubali nyimbo zake.
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wametilia shaka tattoo ya mrembo huyo wakihoji kuwa heunda Diana B amemlipa mrembo achore tattoo yenye uso wake mgongoni kama njia ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari.