You are currently viewing DIANA B AKUTANA NA ALIYECHORA TATTOO YAKE

DIANA B AKUTANA NA ALIYECHORA TATTOO YAKE

Mke wa msanii Bahati na YouTuber maarufu nchini Kenya, Diana Marua amekutana na Rose Waithera ambaye alivuma mtandaoni baada ya kuchora tattoo ya Diana kwenye mgongo wake.

Baada ya wiki kadhaa hatimaye Diana alimtembelea mwanafunzi huyo wa chuo cha urembo katika mtaa wa Githurai na kufanya naye mazungumzo.

Waithera amesema aliamua kuchora tattoo ya mama huyo wa watoto wawili kwa kuwa anamshabikia sana na huwa anatamani kuwa kama yeye.

“Huwa napenda haiba yako, napenda sifa zako, huwa natamani kuwa kama wewe, uko na nyumba ya kifahari, uko na mume mzuri mwenye anakupamba kila wakati, uko na watoto wazuri. Sijawahi kupata mtu yupo na roho kama yako, ningependa kuwa kama wewe, nakupenda,” Waithera alimwambia Diana.

Mwanadada huyo amesema alianza mipango ya kuchorwa tattoo hiyo Desemba mwaka jana, huku akiri kwamba alikosolewa sana baada ya kuchorwa tattoo hiyo ila hana majuto yoyote kwa kile alichofanya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke