Mwanamitandao aliyegeukia Muziki nchini Diana B amelamba dili la nono la kuwa balozi mpya wa kampuni ya bidhaa za urembo iitwayo Phoina Beauty Cosmetics.
Diana B ameshare habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza kwamba ana furaha kujiunga na familia ya Phoina Beauty Cosmetics.
Kwa mafanikio hayo Diana B atatakiwa kutangaza na kuwashawishi wafuasi wake wazinunue bidhaa hizo za urembo wa ngozi za Phoina Beauty Cosmetics kupitia mitandao yake ya kijamii.
Bado haijajulikana amelipwa kiasi gani kwa kuitangaza bidhaa hiyo lakini Diana B sio mgeni katika uteuzi wa kuwa balozi wa bidhaa za makampuni kwani mwaka wa 2021 alilamba shavu ya kuwa balozi wa kampuni ya Unga wa ugali wa Raha Premium.
Hata hivyo mashabiki zake wameonekana kumpongeza kwa mafanikio hayo huku wengine wakitilia shaka ubalozi wake huo na kampuni ya Phoina Beauty Cosmetics ikizingatiwa kuwa balozi wa kwanza wa kampuni hiyo Amber Ray aliingia kwenye ugomvi mzito na mmiliki wa Phoina Beauty Cosmetics kutokana na ishu ya malipo.