Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana B amevunja kimya chake mara baada ya mume wake ambaye ni mgombea wa kiti cha ubunge Mathare Kevin Bahati kufukuzwa kwenye mkutano wa kisiasa wa Azimio la umoja huko Embakasi Mashariki, jijini Nairobi.
Kupitia Instagram yake Diana B amempa moyo mume wake kwa kusema kwamba aendelee kuipigania ndoto yake kuwa mbunge kwa kuwa wapinzani wameanza kuingiwa na uoga kiasi cha kuanza kumpiga vita kwenye azma yake ya kuwa mbunge wa mathare baada ya uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu.
“You are a force that cannot be ignored!!! The way to the top can never be reached without opposition. keep pushing… God got you, Mathare people already know who is best for them,” Amesema Diana B
Kwa upande wake Bahati ameeleza kuwa wapinzani wake waliumizwa na uwepo wake kwenye mkutano huo wa Kisiasa ndiposa wakaamua kufukuza.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Adhiambo amedai kuwa waliokuwa wanasimamia mkutano huo walilazimika kusitisha mkutano ghafla licha ya watu kumtaka awahutubie.
Hata hivyo katibu wa ODM Edwin Sifuna amesisitiza kuwa mgombea wao wa kiti cha ubunge mathare kupitia azimio la umoja ni Anthony Oluoch, hivyo bahati aache kutumia jina lake kutafuta kiki kwani akuhusika kivyovyote kumshurutisha ajiondoe kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare.