You are currently viewing DIANA B AMTUHUMU WILLY PAUL KWA KUMBAKA NA KUMDHALALISHA

DIANA B AMTUHUMU WILLY PAUL KWA KUMBAKA NA KUMDHALALISHA

Mke wa msanii Bahati, Diana Marua amejitokeza hadharani na kusimulia masaibu ambayo alipitia mikononi mwa mwanamuziki mwenye utata Willy Paul.

Kulingana na Diana, kuna kipindi Willy Paul alikuwa anamtaka kimapenzi lakini alipokataa ombi lake, msanii huyo siku moja alimrubuni na kumwingiza kwenye gari  kwa nguvu ambapo alifunga milango na akaondoka kwa kasi huku akiwasha muziki kwa sauti ya juu.

Hitmaker huyo wa “One Day” amesema Willy Paul alimpeleka kwenye nyumba moja ambayo anadai alijaribu kumbaka lakini alifanikiwa kutoka nje ya nyumba hiyo akiwa na nguo zilizochanika ambapo amedai aliokolewa  na mhudumu wa boda boda.

Mama huyo wa watoto wawili amesema ilimchukua miaka 3 kumwambia mume wake Bahati kuhusu kisa hicho, na kilichomfanya azungumze hadharani kwa umma ni hatua ya Willy Paul kuachia diss-track siku chache zilizopita akidai kuwa alitoka nae kimapenzi.

Hata hivyo amesema tayari amefungulia mashataka Willy Paul kwa tuhuma za kumnyanyasa kingono na amehapa kupigania kesi hiyo hadi pale itakapotendewa haki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke