You are currently viewing Diana B ashindwa kuficha hisia zake kwa mume wake Bahati

Diana B ashindwa kuficha hisia zake kwa mume wake Bahati

Mwanamitandao aliyegeukia muziki nchini Diana B ameamua kuwapa somo wanawake wa Kenya jinsi ya kuwaonyesha upendo wapenzi zao.

Mama huyo wa watoto watatu ameshea video hii kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anamlisha mume wake Bahati ambaye kwa sasa anaumwa.

Kwenye posti yake hiyo ameandika ujumbe mzito wa mahaba kwenda kwa mume wake huyo ambaye alionekana kudeka na kitendo hicho huku akimhakikishia kumpenda kwa shida na raha.

“In Sickness and in Good Health, Mapenzi Tight kama kifuniko ya gas “, Aliandika.

Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kukoshwa na upendo wa wawili hao huku wengi wakiahapa kufuta nyayo zao kwa ajili ya kuboresha mahusiano yao.

“Mapenzi wewe any time I pass through dee and bahaa…. I feel I need a man in my life… 2023 wewe lazima mr right akuwe nimechokaa kuangalia ya wenyewe,” Mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii aliandika.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke