Youtuber kutoka nchini Kenya ambaye pia ni rapa Diana B, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ishu ya kupata mtoto wa tatu na mume wake Kevin Bahati.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Diana B amesema sio mbaya akimpata mtoto mwingine huku akisisitiza kwamba watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.
Bi Marua pia ameweka wazi kuwa kupata mtoto mwingine itakuwa zawadi bora zaidi kwa mumewe Bahati ambaye pia ni mwanamuziki.
“Ikiwa kuna mtoto mwingine anakuja, ni sawa. Watoto ni baraka na nikiongeza kifungu kingine katika familia yangu, na nadhani hiyo ndiyo baraka bora zaidi ninayoweza kumpa mume wangu Bahati,” alisema Diana.
Kauli ya Diana B imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa huenda rapa huyo ana uja uzito na anatarajia kupata mtoto katika siku za hivi karibuni.