Watumiaji wa mitandao ya kijamii wametoa maoni mbali kuhusu video ya Diana Marua akiri hadharani kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kwa ajili ya pesa.
Diana alichapisha video hiyo mwaka 2020 mtandaoni ambapo alidai kwamba kabla ya kukutana na mume wake Bahati alikuwa anachepuka na wanaume wengi kwa lengo la kukidhi mahitaji yake ya msingi.
Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi ana umri wa miaka 20 pesa haikuwa shida kwake kwani kila mwanaume aliyekuwa kwenye mahusiano naye alikuwa anamhudumia ipasavyo ikiwemo kumlipia kodi sambamba na kumnunulia chakula na mavazi.
“I dated guys for money I had people who used to give me 10k, kuna mtu anakupatia 30k, anakupea 20k, nilikuwa na mtu wa kunifanyai shopping ya nyumba , nilikuwa na mtu wa kuni buyia manguo , unajua All I wanted was to live well..”, Alisema
Video hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii imeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya ambapo wengi wamehoji kuwa Diana B bado ana tamaa ya pesa na huenda akamkimbia bahati ikitokea amefilisika kiuchumi.
Hata hivyo wengine wamesema kuwa watu waache kumhukumu mwanamama huyo wa watoto watatu kwa kuwa amebadili mienendo yake ya zamani ikizingatiwa kuwa ametulia na analea familia ya mwimbaji huyo.