You are currently viewing DIANA BAHATI AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI LEBO YA MUZIKI YA DIANA B ENTERTAINMENT

DIANA BAHATI AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI LEBO YA MUZIKI YA DIANA B ENTERTAINMENT

Mwanamitandao aliyegeukia muziki nchini Diana Bahati amemtambulisha msanii wake mpya wake mpya anayekwenda kwa jina la Vinny fleva.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Diana B amesema vinny flava atakuwa chini ya lebo yake ya muziki ya Diana B Entertainment ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki huku akiwataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo  ambayo kwa mujibu wake anakuja kubadilisha tasnia ya muziki nchini Kenya.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofauti kimawazo na diana b ambapo wengi wamehoji amemuiga staa wa muziki nchini Nadia Mukami ambaye juzi kati alimtambulisha msanii wake aitwaye Latinoh chini lebo yake ya Sevens Hub Creative.

Tayari Diana B ameachia wimbo wake mpya uitwao “Mubaba” ambao amemshirikisha msanii wake vinny fleva. Wimbo huo ni watatu kwa Diana B tangu aanze career yake ya muziki baada ya one day na Tuachana tu ambazo aliziachia mwishoni mwaka wa 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke