Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana Bahati ametokea kwenye orodha ya wasanii wa kike walio na subscribers wengi barani Afrika.
Kwa mujibu wa The Top Chart, Diana B anashikilia nafasi ya 8 akiwa na jumla ya subscribers elfu 783 nyuma ya Zuchu, Yemi Alade, Sinach, Tiwa Savage, Simi na Nandy ambao wanaongoza kwa idadi ya subscribers kwa wasanii wa kike barani Afrika.
Kwa matokeo hayo Diana B ndiye msanii anayeongoza nchini kwa idadi ya subscribers kwenye mtandao wa Youtube kwa upande wasanii wa wakike.
Diana B ambaye alijiunga na mtandao wa youtube Agosti 19 mwaka 2019, mpaka sasa ana jumla ya watazamaji millioni 119, 452, 136 kupitia kazi zake ambazo anazipakia kwenye mtandao huo.