Msanii Diana Marua amefunguka kwa mara ya kwanza baaada ya watu kumkosoa mtandaoni kwa kuvalia vazi la Balenciaga licha ya kampuni hiyo kupata ukosoaji mkubwa kutokana na kufanya matangazo ambayo yanakiuka maadili ya watoto.
Akizungumza na mume wake Bahati, Diana amesema kuwa hakuwa na ufahamu kuwa chapa ya Balenciaga ilikuwa na utata na ndio maana alivalia vazi lao akiwa tu kwenye shughuli zake za kawaida.
Aidha bahati amemtaka awe makini anapochagua mavazi ya kuvaa kwani huenda ikamleta shida mitandaoni ikizingatiwa kuwa kuna baadhi ya makampuni ambayo hufanya matangazo ambayo yanakwenda kinyume na maadili ya jamii.
Utakumbuka kampuni ya Balenciaga iliomba msamaha juu ya matangazo yenye baada ya kufanya photoshoot ya bidhaa zao mpya ambayo inadaiwa kuendekeza maudhui ya ponografia kwa watoto.