You are currently viewing DIANA MARUA AFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL YOUTUBE

DIANA MARUA AFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL YOUTUBE

Mwanamitandao aliyegeukia muziki  Diana Marua amefuta video aliyotengeneza akidai kuwa staa wa muziki nchini Willy Paul alijaribu kumbaka.

Hii ni baada ya  mahakama ya Milimani kutoa amri  ikimtaka Diana Marua kufuta video ambayo alipakia YouTube mnamo Desemba 9  yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’ ikielezwa kuwa madai yake yameathiri kazi na afya ya Willy Paul .

“Inaamriwa kuwa video ya mshtakiwa/mlalamikiwa na chapisho la mitandao ya kijamii lililochapishwa kwenye chaneli yake ya YouTube yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’, lfutwe ikusubiriwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake kwa vile linamuathiri mlalamishi, kumfanya apoteze fursa za biashara na kumfanya ateseke kiafya” Karatasi ya amri za mahakama iliyotiwa saini na hakimu mkuu mwandamizi D.W Mburu ilisomeka.

Mahakama pia ilimtahadharisha Diana na washirika wake dhidi ya kumharibia jina Willy Paul ikisubiriwa kusikilizwa kwa kesi aliyowasilisha mahakamani. Onyo kali imetolewa kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ya mahakama ambayo ilitolewa tarehe 29 Desemba.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke