You are currently viewing Diana Marua akashifiwa mtandaoni kwa kuvalia vazi la kampuni ya Balenciaga

Diana Marua akashifiwa mtandaoni kwa kuvalia vazi la kampuni ya Balenciaga

Mwanamitandao na msanii Diana Marua amekumbana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wake kwa kuvalia vazi la kampuni ya Balenciaga kipindi hiki ambacho kampuni hiyo inakabiliwa na kashfa nzito ya tangazo lenye utata.

Katika video aliyopakia kwenye mitandao ya kijamii, Diana Marua alionekana jikoni akiangalia chajio  siku ya Jamhuri ambayo mfanyikazi wake wa nyumba alikuwa akiandaa.

Mashabiki wake hata hivyo waligundua amevalia T-shati yenye michoro ua kampuni ya Balenciaga jambo ambalo liliwafanya watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kushangaa kwa nini mwanamama huyo alivaa bidhaa ya kampuni hiyo wakati huu inaendelea kupata ukosoaji mkubwa duniani.

Watu mashuhuri na mashabiki kote ulimwenguni wametangaza hadharani kuachana na Balenciaga  kutokana na kampeni ya aibu ambayo imepelekea watu wengi kupakia video kwenye mitandao ya kijamii, wakichoma bidhaa za Balenciaga

Ikumbukwe Balenciaga inakabiliwa na kashfa ya kufanya photoshoot ya bidhaa zao mpya ambayo inadaiwa kuendekeza maudhui ya ponografia kwa watoto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke