You are currently viewing Diddy akingia kifua Yung Miami baada ya kuitwa mchepuko wake

Diddy akingia kifua Yung Miami baada ya kuitwa mchepuko wake

Baada ya Rapa Diddy kutangaza kuwa amepata mtoto wa kike, DJ Akademiks ameanzisha mjadala kupitia mtandao wa Twitter kuhusu uhusiano uliopo kati ya rapa huyo na mpenzi wake Yung Miami akidai kuwa Miami ni mpango wa kando wa Diddy baada ya kugundua sio mama wa mtoto huyo.

Suala hilo halikumpendeza hata kidogo Diddy ambaye pia ametumia ukurasa wake wa Twitter kujibu kinacho endelea kwa kusema kuwa Yung Miami sio mchepuko wake,hajawahi na hatokua kwa kuwa ni mtu muhimu na wa kipekee kwake.

“@yungmiami305 is not my side chick. Never has been, never will be. She’s very important and special to me, and I don’t play about my Shawty Wop. I don’t discuss things on the internet and I will not start today”, Aliandika.

Mpaka sasa Mama wa mtoto wa Diddy hajawekwa wazi ni lini walibarikiwa kumpata mtoto lakini fununu za ndani zinadai kuwa mtoto huyo ambaye ni wa saba kwa Diddy alizaliwa mwezi Oktoba mwaka huu katika hospitali ya Newport Beach, California.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke