You are currently viewing DIDDY AMPA JAY Z MAUA YAKE AKIWA HAI,AMFANANISHA NA TUPAC PAMOJA NA BIGGIE

DIDDY AMPA JAY Z MAUA YAKE AKIWA HAI,AMFANANISHA NA TUPAC PAMOJA NA BIGGIE

Rapa kutoka Marekani P.Diddy ameamua kumpa Jay-Z maua yake akiwa angali hai.

Bosi huyo wa lebo ya muziki ya “Love Records” amempongeza kwa kusema kwamba amefanikwa kuvaa viatu vya manguli wawili wa Hip Hop duniani, marehemu Tupac Shakur na Notorious B.I.G.

Diddy amesema hayo kupitia Twitter Spaces iliyowakutanisha pamoja na Fat Joe kwenye Kumbukumbu ya miaka 50 ya Kuzaliwa kwa marehemu Notorious B.I.G.

Utakumbuka Mei 21 mashabiki wa muziki wa HipHop duniani walisherekea kwa masikitiko kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Marehemu Notorious B.I.G. ambaye alizaliwa Mei 21 mwaka 1972.

Notorious B.I.G. aliuawa Machi 9 mwaka 1997 akiwa kwenye gari lake na watu wengine wakati wakitoka kwenye sherehe ya tuzo za Soul Train huko Los Angles nchini Marekani.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke