You are currently viewing DIDDY KUPOKEZWA TUZO YA MAFANIKIO YA MAISHA BET 2022

DIDDY KUPOKEZWA TUZO YA MAFANIKIO YA MAISHA BET 2022

Msanii wa Hip Hop Marekani, Sean Combs maarufu kama Diddy anatarajiwa kupokea Tuzo ya Heshima na Mafanikio ya Maisha kutoka BET zinazotarajiwa kutolewa Juni 26, 2022 katika ukumbi wa Microsoft Theater Jijini Los Angeles, Marekani.

Tuzo hizi zinaandaliwa na Black Entertainment Television (BET) toka Juni 19, 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo.

“Ni heshima kuwa sana kwa tasnia ambapo sio tu ametengeneza utamaduni kupitia kazi zake, lakini pia amekuwa kiongozi katika mabadiliko ambayo mara kwa mara yanahusisha vizazi kwa vizazi na kuchangia kuongeza ubora kwennye tasnia yetu hivyo anastahiki hili,” wamesema BET

Ikumbukwe wasanii wa kwanza kukabidhiwa tuzo ya BET ni kundi la Outkast liloundwa mwaka 1992 na wasanii wawili (Andre ‘3000’ Benjamin na Antwan ‘Big Boi’ Patton) ambapo mwaka 2001 walishinda katika kipengele cha Best Group.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke