You are currently viewing Didy atangazwa kuwa Billionea

Didy atangazwa kuwa Billionea

Rapa mkongwe na Mfanyabiashara kutoka Marekani Diddy ametangazwa rasmi kufikia hadhi ya Bilionea. Kwenye orodha mpya ya Hip Hop Rich List ambayo imetolewa na mhariri wa zamani wa jarida la Forbes Zack O’Malley, imemtaja Diddy kuwa ana utajiri wa billioni 121 za Kenya.

Hiyo inamfanya Diddy kuwa rapa wa pili tajiri zaidi duniani, nyuma ya Jay-Z ambaye utajiri wake ni billioni 182, kilichomfikisha Diddy kwenye kiti hicho ni uwekezaji wake wa muda mrefu kupitia kinywaji cha Ciroc, DeLeon tequila lakini pia kampuni yake ya Revolt.

Orodha hiyo imemtupa nje Kanye West ambaye wiki hii alitangazwa kuikosa hadhi ya Bilionea baada ya utajiri wake kushuka na kufikia billioni 48 kufuatia kuvunjika kwa ndoa yake na Adidas.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke