Moja kati ya waongozaji maarufu wa video za muziki nchini Tanzania Director Joowzey, ametoa maoni yake kuhusu video mpya ya “I Miss You” ya mwanamuziki Rayvanny.
Joowzey ambaye ameongoza video za wanamuziki mbalimbali kama Whozu, Aslay ,na Mabantu, amedai kuwa kwa asilimia kubwa script na stori kuhusu video ni nzuri na vimefanyika kwa usahihi lakini upande wa rangi iliyotumika katika video hiyo haikua sahihi, hii ni kutokana na director Ivan aliyeongoza video hiyo kumtegemea mtu mwingine katika upande wa rangi.
Kauli yake imekuja mara baada ya Rayvanny kujinadia kuwa video ya wimbo wake wa “I Miss You” aliyomshirikisha Zuchu ndio video ghali zaidi kuwahi kutayarisha nchini Tanzania ikizingatiwa kuwa ilimgharimu kiasi cha shillingi millioni 80 za Tanzania.