DJ Khaled ametangaza rasmi jina la Album yake mpya ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Khaled amesema Album hiyo ameipa jina la “GOD DID” na ni mahususi kwa ajili ya wanaoamini na wasioamini Mungu.
“GOD DID”☝🏽 THE OFFICIAL ALBUM TITLE FOR MY 13TH STUDIO ALBUM
COMING SOON
I made this album for all the believers and non believers. They didn’t believe in us…do you? 🫵🏽 #GODDID” Ameandika Instagram.
Licha ya kututajia jina la album yake mpya, DJ Khaled hajaweka wazi idadi ya nyimbo wala wasanii aliowashirikisha kwenye album yake hiyo ila ni jambo la kusubiriwa.
“GOD DID” itakuwa ni Album ya 13 kutoka Studio kwa mtu mzima DJ Khaled ikiifuata ‘Khaled Khaled’ ya mwaka 2021 ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju 20 ya moto.