You are currently viewing DJ KHALED KUTUNUKIWA NYOTA KWENYE HOLLYWOOD WALK OF FAME

DJ KHALED KUTUNUKIWA NYOTA KWENYE HOLLYWOOD WALK OF FAME

Mtayarishaji wa muziki na Dejaay maarufu kutoka nchini Marekani DJ Khaled ataungana na mastaa wengine wakubwa duniani waliopewa heshima ya kutunukiwa nyota kwenye Hollywood Walk of Fame.

Kwa mujibu wa mtandao wa Variety, Khaled atatunukiwa nyota hiyo April 11, mwaka huu.

Dj khaled amewahi kushinda tuzo za Grammy mara moja, ni mwandishi wa nyimbo na ni mtayarishaji wa muziki. Ametajwa kuwa atatunukiwa nyota hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 18.

Utakumbuka, Hollywood Walk of Fame ni eneo la kutembea kwa miguu kando kando ya majengo katika eneo la Hollywood ambapo nyota za watu waliofanya vyema kwenye upande wa burudani zimewekwa. Walengwa ni wanamuziki, waigizaji, waelekezi wa filamu, watayarishaji wa muziki na filamu na makundi ya waigizaji.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke