You are currently viewing DJ ROJA AKANUSHA TUHUMA ZA KUKIMBIA NA MKE WA MTU

DJ ROJA AKANUSHA TUHUMA ZA KUKIMBIA NA MKE WA MTU

Msanii ambaye pia DJ maarufu nchini DJ Roja amekanusha tuhuma za kumpokonya shabiki mke  akiwa anakula bata kwenye bar iitwayo Plot 8 huko Kololo viungani mwa jiji la Kampala.

Roja amesema madai hayo hayana ukweli wowote na hivyo mashabiki zakr wasichukulia kwa uzito taarifa hizo za kutoroka na mke wa mtu kwani mara ya mwisho kufanya kazi Plot 8 bar ilikuwa ni miezi mitano iliyopita.

Hata hivyo ameonekana kuchukizwa na madai hayo kwa kusema kwamba mwanaume aliyoibua tuhuma hizo alikuwa anataka kuipaka tope brandy yake lakini pia kutumia jina lake kujitafutia umaarufu mtandaoni.

Kauli ya DJ Roja imekuwa mara baada ya mwanaume mmoja mapema wiki kujitokeza na kumsuta vikali dj huyo kwa kumpokonya mke wakiwa wanajiburudisha huko Kololo nchini uganda ambapo alienda mbali zaidi na kusema kwamba anamsaka DJ huyo ili amrudishie mke wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke