Dj Rasmi wa Harmonize, DJ Seven yupo mbioni kuachia Extended Playlist (EP) yake mpya iitwayo “GREATNESS”
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameachia tracklist ya EP yake hiyo ambayo ina jumla ya nyimbo 6 huku zote zikiwa kolabo.
Kwenye EP hiyo DJ Seven amewashirikisha wasanii kama Jose Chameleone, Killy, Dulla Makabila, Weasel, Daddy Andrea, Malaika na Balaa MC.
Licha kutoweka wazi siku ambayo hiyo itaingia sokoni amewataka mashabiki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kupokea Greatness EP