Kipindi maarufu cha televisheni cha Househelps of Kawangware kimerejea hewani na mashabiki wamegundua kuwa Dj Shiti si miongoni mwa waigizaji walioshirikishwa kwenye msimu mpya wa kipindi hicho.
Akizungumza katika mahojiano hivi karibuni, DJ Shiti amesema ameshikika na majukumu mengi ya kikazi nje ya Nairobi kwa kufanya kazi katika miradi tofauti, katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma huko Turkana ambayo huenda iliathiri uwepo wake katika msimu mpya wa Househelps of Kawangware.
DJ Shiti hata hivyo ameahidi kwamba atarejea hivi karibuni kwenye kipindi hicho.
“Ni shoo kubwa na mashabiki wangu watarajie kuniona hivi karibuni. Bado nitakuwa Shiti yule yule mzee ambaye hadhira inampenda.”, Alisema.
Mchekeshaji huyo amesema anakosa umoja na undugu alioshirikiana na waigizaji wenzake walipokuwa wakifanya kazi pamoja.
Househelps of Kawangware ni kipindi ambacho inaangazia maisha ya wafanyakazi wa nyumbani na mwingiliano wao wa kila siku na marafiki wakiwa kwenye harakati zao za maisha.