You are currently viewing DJ SHITI AMCHANA BABY MAMA WAKE KUPITIA DISS-TRACK “DRAMA ZA MAMA MIRIAM”

DJ SHITI AMCHANA BABY MAMA WAKE KUPITIA DISS-TRACK “DRAMA ZA MAMA MIRIAM”

Mchekeshaji maarufu nchini DJ Shiti ameachIa diss-track iitwayo Drama za Mama Miriam akiwa amemshirikisha Sadii, Diss-track ambayo amemchana baby mama wake ambaye juzi kati alimsuta vikali kwa hatua ya kumtelekeza mtoto wao.

Kwenye diss-track hiyo DJ Shiti amesikika kwenye moja ya mashairi akimchana baby mama wake huyo kwa kumtaka aache kumharibia jina ikizingatiwa kuwa kipindi alikuwa amevulia kiuchumi hakuna mtu yeyote alitaka kujihusisha nae.

Lakini pia amewachana mablogger na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaoneza uvumi dhidi yake ambapo amewataka wasiwe wepesi wa kueneza taarifa zisizo kuwa na kweli.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumubeza dj shiti kwa kuachia diss track kwenda kwa baby wake huyo wakisema mwanaume rijali hana muda ya kujibishana na wanawake huku wengine wakienda mbali zaidi na kuhoji kuwa huenda mchekeshaji huyo anatumia jambo hilo kama kiki ili azungumziwe kwenye vyombo vya habari nchini bada ya kumtambulisha msanii wake Sadii.

Utakumbuka wiki iliyopita mwanamke mmoja kwenye mtandao wa Instagram aliibuka kupitia insta story yake na kumtupia DJ Shiti kila aina matusi kwa kumtelekeza mtoto wao kwani amekuwa akituma shillingi 150 kwa ajili ya matunzo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke