Sehemu ya tatu (3) ya filamu iliyojaa maisha ya Rapa kutoka nchini Marekani Kanye West iitwayo “Jeen-Yuhs” inatarajiwa kuzinduliwa Machi 2, Mwaka wa 2022 katika mtandao wa NetFlix.
Filamu hiyo imetengenezwa kwa kuunganisha vipande vya video alizorekodiwa na marafiki zake waliokuwa wanamfatilia kwa takribani miaka 20.
Matukio yaliyojumuishwa kwenye filamu hii ni kama kifo cha mama yake, Donda na matatizo yake ya afya ya akili pamoja na mchakato wake wa kugombea uraisi ulivyofeli.
Documentary Hiyo Imeandaliwa na Waliokuwa Waongozaji Wa Video Za nyimbo mbili za Kanye West Jesus Walk na Through The Wire ambao ni Director Chike Ozah Pamoja na Clarence Simons.
Hivyo Documentary ya Jeen-Yuhs Inatarajiwa Kuanza Kuonekana kwenye mtandao wa Netflix Machi 2 mwaka wa 2022.