You are currently viewing Dogo Richie akiri kwenda kwa mganga kusafisha nyota yake ya muziki

Dogo Richie akiri kwenda kwa mganga kusafisha nyota yake ya muziki

Mwanamuziki kutoka Pwani Dogo Richie kwa mara ya kwanza amekiri kuwa aliwahi kwenda kwa mganga ili amsaidie atoke kimuziki.

Katika mahojiano na Presenter Ali Dogo Richie amesema baada ya kufika kwa mganga aliona kuwa hawezi kumsaidia na tangu kipindi hicho aliacha kuamini kwenye masuala ya kishirikina kwani ndio kikwazo kikubwa cha watu wengi kutoendelea kimaisha.

Hitmaker huyo wa “Tule Sheshe” amewaasa watu kutoamini katika imani za kishirikina na badala yake wamgeukie Mungu wanapokumbwa na matatizo katika maisha.

Lakini pia amenyosha maelezo kuhusu suala la kumtamani kimahusiano malkia wa Tiktok Azziad kwa kusema kuwa ana penzi la kweli kwa mrembo huyo na wala hatafuti kiki kama watu wanavyosema mtandaoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke