Msanii kutoka Pwani Dogo Richie ametoa ya moyoni kuhusu mabinti wanaotumia mtego wa mapenzi kuwanyanyasa vijana wa kiume kihisia kwa manufaa yao binafsi.
Kupitia Whatsapp story yake Hitmaker huyo wa “Tule Sheshe” ametoa changamoto kwa watoto wa kike wasile pesa za wanaume ambao hawana hisia nao kama njia ya kupunguza visa vya vijana kujitoa uhai.
Lakini pia amewapa somo vijana wa kiume kwa kuwataka wawakimbie mabinti wanaotumia mahusiano ya kuigiza kama kitega uchumi ya kuwaingizia riziki.
Kauli yake imekuja mara baada kijana mmoja ukanda wa Pwani kujitoa uhai kwa madai ya kusalitiwa kimapenzi na mwanadada aliyekuwa anampenda sana.