Staa wa muziki nchini, Dogo Richie amepata shavu kubwa baada ya kusainiwa katika lebo ya Kaya Records inayomilikiwa na Kaya Media.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa, Dogo Richie amesema ana furaha tele kujiunga na lebo hiyo huku akiwataka mashabiki zake kusubiri mengi makubwa kutoka kwake kwenye safari yake mpya na Kaya Records.
Sanjari na hilo Dogo Richie amesema licha ya kuingia ubia wa kufanya kazi na uongozi mpya, lebo yake ya Reclaim itaendelea na harakati za kuwasaidia vijana kisanaa kwani tayari amewateua watu wapya ambao watasimamia lebo hiyo.
Kaya Records ni moja kati ya lebo kubwa sana za muziki ukanda wa Pwani na ilianzisha mwaka 2021 kwa lengo la kukuza vipaji vya vijana kupitia muziki. Utakumbuka kabla ya Dogo Richie kujiunga na Kaya Records,alikuwa anafanya kazi kwa ukaribu na Dallaz Records.
Kwa sasa Dogo Richie anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Tule Sheshe”, ambao ameuachia chini uongozi wake mpya, Kaya Records.