Mwanamuziki kutoka Kenya Dogo Richie amesema wasanii nchini humo wanawapa Bloggers wakati mgumu kwa kukosa ubunifu na kupanga matukio yatakayo wapa nafasi ya kuzungumziwa katika mitandao ya kijamii.
Kwenye mahojiano ya hivi karibuni Ndogo Richie amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya mashabiki wengi wa mziki hapa nchini kupenda kusoma tarifaa za burudani katika mitandao ya Udaku ya nchini Tanzania.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Bilnaden” amesema kuwa kwa sasa ni vigumu kwa msanii kupata mafanikio makubwa pasi na kuwa na matukio yatakao mfanya awe gumzo kwa mashabiki zake.
Hata hivyo amewapa changamoto wasaani kuwa wabunifu ili kuwapa bloggers maudhui ya burudani yatakayo jenga gumzo kwa mashabiki wao