You are currently viewing DOJA CAT ASITISHA ZIARA YAKE YA MUZIKI KISA UPASUAJI WA KUONDOA TONSIL

DOJA CAT ASITISHA ZIARA YAKE YA MUZIKI KISA UPASUAJI WA KUONDOA TONSIL

Mwanamuziki kutoka Marekani Doja Cat amesitisha ziara yake ya muziki kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tonsil.

Hii ni baada ya mrembo huyo kunywa pombe wakati akiwa kwenye matumizi ya dawa zinazozuia bakteria “antibiotiki”

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe unaosomeka “hi guys nilitamani sana, nilitaka msikie kutoka kwangu kwanza, kwa bahati mbaya natakiwa kufanya upasuaji wa kuondoa tonsil kwa haraka sana.”, Doja Cat Amendika kupitia Instastory yake.

Doja Cat ameendelea kwa kusema kwamba “upasuaji tayari umeshapangwa lakini kupona itachukua muda kidogo, kwasababu ya uvimbe. hii ina maana kwamba natakiwa kusitisha tamasha langu katika kipindi hiki cha msimu wa majira ya joto pamoja na ziara ya theweeknd iitwayo “after hours til dawn”. najiskia vibaya juu ya hili lakin ni lazima nisubiri hili nipone niweze kurejea katika hali yangu ili nitengeneze muziki kwajili yenu wote”, Doja Cat Amesisitiza.

Hii ina maana kwamba Doja Cat hatotokea kwenye tamasha la Hangout mjini Alabama alilokuwa alifanye wikiendi hii pamoja na Glastonbury huko United Kingdom (uk) alilotakiwa kulifanya mwezi Juni mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke