Mwanamuziki kutoka Marekani Doja Cat ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo itakuwa kwenye muundo wa R&B na hato-rap kama alivyozoeleka.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameongeza kwa kusema “Sifanyi album ya kitamaduni za kijerumani…nilikuwa nikitania chombo kimoja cha habari ambacho kilinihoji kuihusu”.
Hii itakuwa album yake ya nne kutoka studio baada ya kutamba na Amala ya mwaka 2018, Hot Pink ya mwaka 2019 na Planet Her ya mwaka 2021. Kabla ya hapo aliwahi kuachia EP mbili ambazo ni Purrr ya mwaka 2014 na Streets Remixes ya mwaka 2021.