You are currently viewing Don Jazzy amzika mama yake baada ya miezi mitatu.

Don Jazzy amzika mama yake baada ya miezi mitatu.

Bosi wa lebo ya rekodi kutoka Nigeria, mtayarishaji wa muziki, msanii wa kurekodi, mshawishi wa vyombo vya habari, na mwanahisani Don Jazzy hatimaye amemzika marehemu mama yake wikiendi hii huku tukio hilo likipambwa na watu wengi mashuhuri.

Mnamo Julai 2022, Don Jazzy alitangaza kwamba alimpoteza mama yake kutokana na saratani, mazishi hayo yalipangwa kufanyika Oktoba 19 na 20, 2022 na badala yake amezikwa tarehe 8/10/2022, lilikuwa tukio la kupendeza huku watu mashuhuri mbalimbali katika tasnia ya burudani wakipamba maziko hayo.

Waliohudhuria walikuwa wanamuziki wa A-list wakiwemo Tiwa Savage, D’banj, Timaya, na washiriki wa zamani na wa sasa wa Mavin records miongoni mwa wengine wengi.

Watu wengine mashuhuri na washiriki wa hafla hiyo ni pamoja na Obi Cubana, Erica wa Big Brother Naija, Pretty Mike, Mwanahabari Dotun, Kenny Ogungbe, Dayo Adeneye, na Warri Pikin.

Tukio lililofanyika The Monarch Lagos Nigeria na wageni walipewa sare zenye maandishi ya Kinigeria (Aso Ebi) ambayo kulingana na Warri Pikin alivyosema, wageni walipokea sare hizo bila malipo kutoka kwa Don Jazzy.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke