You are currently viewing DR. DRE AFIKISHIWA NYARAKA ZA TALAKA AKIWA MAKABURINI.

DR. DRE AFIKISHIWA NYARAKA ZA TALAKA AKIWA MAKABURINI.

Sakata la kuvunjika kwa ndoa ya mtayarishaji mkongwe Dr. Dre bado linashika vichwa vya habari duniani, Sasa jipya limeibuka ambapo tovuti ya TMZ imeripoti kwamba Dre amefikishiwa nyaraka za kisheria kuhusiana na mchakato wa talaka, lakini amefikishiwa nyaraka hizo akiwa makaburini.

Tunaambiwa Dr. Dre alikuwa akimzika Bibi yake ndipo mtu mmoja alipofika na karatasi hizo kisha kumshikisha Dre ambaye alikuwa amesimama kando ya Jeneza. Taarifa zinasema Dre alikasirika kuona kitendo kama hicho.

Tovuti ya TMZ imebaini nyaraka hizo ambazo zilifikishwa kwa Dre zilikuwa zinahusu malipo ya mwanasheria wa aliyekuwa mke wake Bi. Nicole Young kwa ajili ya mchakato huo wa talaka.

Kuna mgogoro wa malipo hayo ambapo Dre alilipa takriban shilling million 36.1 badala ya shilling millioni 175 ambayo inadaiwa kwamba Jaji alipitisha akimtaka Dr. Dre ailipe, hivyo karatasi hizo ni agizo la Jaji.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke