Mahakama imemuamuru mtayarishaji nguli wa muziki duniani Dr. Dre kumlipa aliyekuwa mke wake Nicole Young zaidi ya Shilingi bilioni 11za Kenya baada ya kuvunjika kwa ndoa yao
Kwa mujibu wa Tmz Dr Dre anatakiwa kuanza kulipa kiwango nusu cha pesa hiyo na nyingine kumalizia ndani ya mwaka mmoja.
Hapo awali Nicole Young alitaka agawane mali nusu kwa nusu na mtayarishaji huyo wa muziki lakini mahakama imetengua hilo na kuamuru Dre kulipa kiasi hicho cha pesa.
Nicole atatakiwa kulipa mwenyewe gharama za kuendesha kesi ambazo zinatajwa kuwa mabilioni ya pesa.
Dr Dre na Nicole Young ambao wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 25, tayari wameshapeana talaka