Mchekeshaji Dr. Ofweneke ameshangazwa na kiasi cha pesa alichotakiwa kulipa kwa ajili ya kumleta Burna Boy kutumbuiza nchini Kenya.
Kupitia ukurasa wa Instagram Ofweneke amesema uongozi wa Burna Boy kupitia mama yake mzazi Bose Ogulu ulimtaka alipe kiasi cha shillingi millioni 70 kumpata msanii huyo kutumbuiza kwenye mkesha wa kukaribisha mwaka mpya wa 2023.
“Weeh tried reaching out to the mum for a new year’s event … he is now charging Ksh 70 M,” alisema Dr. Ofweneke.
Hata hivyo kauli hiyo imezua mjadala mzito miongoni watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakitamtaka mchekeshaji huyo kuwapa nafasi wasanii wa Kenya kwenye onesho lake lijalo badala ya kuwazingatiwa wasanii wa nje ambao watamtoza kiasi kikubwa cha pesa.