You are currently viewing DRAKE ADAIWA KUTOKA KIMAPENZI NA KYLIE JENNER

DRAKE ADAIWA KUTOKA KIMAPENZI NA KYLIE JENNER

Urafiki wa Drake na Travis Scott unaweza kuwa hatiani kuanzia sasa kwani Drake anadaiwa kuwa alifanya mapenzi na Kylie Jenner mwaka 2020.

Hii ni kwa mujibu wa baby mama wa Tristan Thompson ambaye kupitia insta story yake alimwaga ubuyu huo.

Maralee Nichols ambaye ana mtoto mmoja na Tristan, alikuwa akimrushia maneno nyota huyo wa NBA ambapo kwenye maneno yake alisema, Tristan anafahamu kila kitu kuhusu Drizzy kulala na Kylie lakini kwa kuwa hajakamilika, hawezi kumwambia Travis Scott.

Tristan ambaye anakipiga katika timu ya mchezo wa kikapu ya Sacramento Kings nchini Marekani aliwahi kuwa penzini na dada yake Kylie Jenner, Khloe Kardashian na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke