You are currently viewing DRAKE ALIPITA NA MREMBO JULIA FOX KABLA YA KANYE WEST

DRAKE ALIPITA NA MREMBO JULIA FOX KABLA YA KANYE WEST

Kumbe Rapa Kanye West kutoka nchini Marekani amepita sehemu ambayo rapa mwenzake Drake alipita kitambo.

Taarifa mpya mjini zinadai kwamba Drake aliwahi kuwa na mahusiano na mrembo Julia Fox ambaye kwa sasa yupo penzini na Kanye West.

Kwa mujibu wa tovuti ya Page Six, penzi lao lilianza mwaka 2020 kufuatia ukaribu ulioanza mwaka 2019 baada ya Drizzy kumtelezea DM mrembo huyo na kumsifia kuhusu ushiriki wake kwenye filamu ya Uncut Gems. Julia Fox aliachana na mumewe Artemiev na Drake ndiye akawa tulizo lake la muda mfupi.

Kumbuka kuwa kipindi cha nyuma kabla ya wawili hawa kuzika tofauti zao walikuwa kwenye bifu zito huku sababu kubwa ikitajwa kuwa Drake aliwahi kusema kuwa yupo kwenye mahusiano na Ex wa rapa Kanye West ambaye ni Kim Kardashian na kwa kuthibitisha hilo alim-follow Instagram pamoja na kutoa ngoma yake ya “In My Feeling” akimuimba “Kiki” ambalo ni jina lingine la mrembo huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke