You are currently viewing DRAKE AWACHEKA FORBES KWA ORODHA YAO YA WASANII WA HIPHOP WALIOINGIZA FEDHA NYINGI 2021

DRAKE AWACHEKA FORBES KWA ORODHA YAO YA WASANII WA HIPHOP WALIOINGIZA FEDHA NYINGI 2021

Rapa kutoka Marekani Drake ameonyesha wazi kuikataa orodha ya wasanii 10 wa Hip Hop walioingiza fedha nyingi kwa mwaka 2021, akitajwa namba 4, Jay-Z akiwa kinara kwenye orodha hiyo.

Kwenye orodha hiyo Drake ametajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 50 kwa mwaka 2021 kitu ambacho ameonesha hajakubaliana na tathmini hiyo.

Drake amewajibu Forbes kwa kuangua kicheko kwa kuweka emoji ya kucheka katika taarifa hiyo kwenye mtandao wa Instagram.

Inaelezwa kuwa watoa tathimini walikosea, kwani mapato ya mkali huyo yanadaiwa kuzidi kiasi cha dola milioni 50 walizoziweka.

Ikumbukwe, Forbes walitoa orodha hiyo  Jumanne ya wiki iliyopita, ikiwa ni utaratibu wake wa kufanya hivyo kila mwaka.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke