You are currently viewing Drake kutoa ushuhuda wa mauji ya Rapa XXXTentacion mwaka

Drake kutoa ushuhuda wa mauji ya Rapa XXXTentacion mwaka

Rapa Drake ni miongoni mwa watu maarufu sita ambao wameorodheshwa kwa ajili ya kutoa ushuhuda kwenye shtaka la mauaji ya Rapa XXXTentacion mwaka 2018 ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi. Mawakili wa utetezi wamewasilisha orodha hiyo yenye jina la Drake, Quavo, Offset, marehemu Takeoff, Tekashi 6ix9ine na Joe Budden ambao wametajwa kama mashahidi kwenye nyaraka hizo za Mahakama.

Drizzy ametajwa kwenye shtaka hilo la mauaji ya XXXTentacion kufuatia bifu lao la mwaka 2017 ambapo marehemu XXX aliwahi kuibuka na kudai Drake ameiba midondoko yake (flows) kutoka kwenye wimbo wake wa kwanza “Look At Me” na kuitumia kwenye wimbo wake “KMT” wa mwaka 2017.

Baada ya mwaka mmoja wa kutupiana maneno na mvutano, akaunti ya Instagram ya XXXTentacion upande wa insta story yaliandikwa maneno yasemayo “If anyone tries to kill me it was Drake,” akimtaja Drizzy kama mtu ambaye anatishia kuchukua uhai wake. Miezi minne baadaye, rapa huyo aliuawa kwa kupigwa risasi mjini Florida.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke