You are currently viewing DRE CALI ATIMKIA CANADA BAADA YA KUZICHAPA NA BOSI WAKE YKEE BENDA

DRE CALI ATIMKIA CANADA BAADA YA KUZICHAPA NA BOSI WAKE YKEE BENDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda, Dre Cali ameripotiwa kutimkia nchini Canada baada ya kuzichapa na msanii Ykee Benda ambaye ni bosi wa lebo ya muziki ya Mpaka Records inayosimamia kazi zake za muziki.

Inadaiwa wawili hao walirushiana makonde baada ya kuingia kwenye ugomvi mkali wa pesa, jambo lilompelekea Dre Cali kwenda mafichoni nchini Canada kwa ajili ya usalama wake.

Chanzo cha karibu na Dre Cali kimeuambia mtandao wa Howwe kuwa msanii huyo alidanganya kuwa anasafiri nchini Canada kufanya shows hadi akapewa hatia ya usafiri ya miaka 10 ila kiuhalisia lengo lake kuu lilikuwa apate visa ya kwenda mafichoni.

Utakumbuka Dre. Cali pia anaandamwa na msala mwingine wa kukiuka mkataba wake wa miaka 5 na menejimenti yake ya zamani ya “Wyse Technologies Limited” mwaka 2018 kabla ya kuijiunga na lebo ya “Mpaka Records” inayomilikiwa na msanii Ykee Benda.

Kwa sasa uongozi wake wa zamani “Wyse Technologies Limited” unamtaka Dre Cali alipe fidia ya Shillingi laki 8 za Kenya kwa hasara aliyoiletea menejimenti yake hiyo huku ikisisitiza kuwa haitalegeza msimamo wake hadi pale watakapopata haki mahakamani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke