You are currently viewing DRE CALI HATIANI KWA KUKIUKA MKATABA WAKE NA WYSE TECHNOLOGIES LIMITED

DRE CALI HATIANI KWA KUKIUKA MKATABA WAKE NA WYSE TECHNOLOGIES LIMITED

MMsanii wa Mpaka Records Dre Cali yuko matatani baada ya uongozi wake wa zamani wa Wyse Technologies Limited kutishia kufungulia mashtaka kwa kukiuka mkataba wa maelewano.

Kulingana na barua na kutoka kwa Wyse Technologies, Dre Cali anaripotiwa kukiuka mkataba wa miaka 5 ambao alikubaliana na uongozi wake huo kwa lengo la kukuza kipaji chake cha muziki.

Barua hiyo, inasema kwamba Dre Cali, ambaye kwa wakati huo alikuwa anaitwa ‘Drey 23’, alitia saini kandarasi hiyo ambayo ingedumu kwa kipindi cha  miaka mitano kuanzia Machi 27, 2018 hadi Machi 27, 2023.

Barua hiyo iliendelea kusomeka kuwa akiwa amekaa takribani miezi mitano tu chini ya uongozi wake wa zamani , Dre aliachana na uongozi huo na kujiunga na lebo ya Mpaka Records bila kufuata taratibu stahiki

Kulingana na duru za kuaminika, Wyse technologies imemtaka Dre Cali kuwalipa takriban shillingi laki nane kama fidia.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke