Mwanamuziki wa dancehall nchini Dufla Diligon ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia ndani ya mwaka huu wa 2022.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Dufla amethibitisha ujio wa ep hiyo kwa kusema kwamba anaendelea na mchakato wa kuandaa ep mpya huku akiwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea EP yake hiyo.
Hata hivyo hajeweka wazi Idadi ya ngoma wala tarehe rasmi ambayo EP yenyewe itaingia sokoni ila amedokeza ujio wa kolabo yake na Visita ambayo ataachia muda wowote kuanzia sasa.
Hii inaenda kuwa EP ya kwanza kwa mtu mzima Dufla Diligon tangu aanze safari yake ya muziki.