You are currently viewing DUFLA DILIGON AZUA GUMZO MTANDAONI, AKIRI KUWA BABA WA MTOTO WA CAROL SONIE

DUFLA DILIGON AZUA GUMZO MTANDAONI, AKIRI KUWA BABA WA MTOTO WA CAROL SONIE

Mwanamuziki wa Dancehall nchini Dufla Diligon ameingia kwenye headlines mara baada ya kukiri kuwa baba wa mtoto wa Carol Sonie ambaye ni mpenzi wa zamani mchekeshaji Mulamwah.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Dufla amesema aliumizwa na kitendo cha Mulamwah kumkana hadharani mtoto huyo huku akisema kwamba yupo tayari kutoa matunzo kwa mtoto wa Carol Sonie kwani wana ukaribu na mrembo huyo.

“Namjua Caro na siwezi taka kuongelea mambo mob sahi kwa sababu Mulamwah amewaka sana na hiyo stori ni moto. Niliona Mulamwah alikataa mtoto lakini mimi siwezi kataa huyo mtoto naweza mchukua ni msaidie. Mi am ready kumchukua, kumsaidia na mama yake. Sonnie ni mabeshte .. ” Alisema

Dufla Diligon ameweka wazi hayo mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa huenda msanii huyo ndiye baba ya mtoto wa Carol Sonie kutokana na picha yake na mrembo huyo kusambaa mitandaoni wiki kadhaa zilizopita.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke