You are currently viewing DULLY SYKES: STAREHE ILIWAPONZA WASANII WA ZAMANI WA BONGOFLEVA

DULLY SYKES: STAREHE ILIWAPONZA WASANII WA ZAMANI WA BONGOFLEVA

Mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes anasema kuwa, sababu za wasanii wengi wa zamani kufulia au kutofanikiwa kulitokana na kuendekeza starehe.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Dully anasema kuwa, zamani wasanii walikuwa wanapata pesa japokuwa hazikuwa nyingi kama wanazopata wasanii wa sasa, lakini walikuwa wanashindwa kufanya vitu vya maana zaidi ya starehe.

“Tulikuwa tunapata pesa ambazo kama tungetumia akili ya kuzidunduliza tungeweza kununua viwanja vitatu hata vinne ambavyo kwa miaka ya sasa mtu angeweza kuuza hata kimoja tu ukajenga nyumba, lakini hatukufanya hivyo zaidi sana pesa ziliishia kufanya starehe,” anasema na kuongeza;

“Hata ukifuatilia nyimbo zetu tulizokuwa tunaimba zamani zilikuwa zinahamasisha starehe, kula vizuri na kuvaa vizuri tofauti na sasa ndoto za wasanii wengi ni kujenga nyumba na kumiliki magari mazuri.”

Dully anasema pesa walizokuwa wanapata kipindi hicho cha nyuma zilikuwa zinawatosha, lakini zilikuwa hazina matumizi sahihi hivyo wakongwe hawatakiwi kuwa na sababu kwamba walikuwa hawapati pesa na kufanya mambo makubwa.

Mkali huyo wa ngoma ya Salome anasema kuwa, hakuna pesa ndogo, bali muhimu ni kuwa na malengo na utafanikiwa tu

 

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke