You are currently viewing EDDY KENZO AAPA KUMALIZA UGOMVI WA KING SAHA NA BEBE COOL

EDDY KENZO AAPA KUMALIZA UGOMVI WA KING SAHA NA BEBE COOL

Staa wa muziki nchini Uganda,Eddy Kenzo amefichua kuwa ugomvi unaoendelea kati ya Bebe Cool na King Saha unamchukiza.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema wasaniii wanapaswa kuacha kutupiana maneno makali mtandaoni na badala yake waungane kwa ajili kuupeleka muziki wà Uganda kimataifa.

“I hate the negativity in this industry. I don’t like artists who fight each other. We don’t need a divided industry. We need to grow first and conquer the international market,” Amesema

Eddy kenzo ameahidi kuwaleta pamoja King Saha na Bebe Cool ambao wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu kwa kuwa ni marafiki zake.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” ameeleza kuwa tasnia ya muziki nchini Uganda bado ni changa hivyo wasanii wanapaswa kuelekeza nguvu zao kubuni njia za kuingiza kipato na kutoa muziki mzuri badala kupigana vita.

“I will work to unite the two because I speak to both. Artists ought to know our industry is still young, we should unite and fight brokenness instead of fighting one another,”  Ameongeza

King Saha na Bebe Cool wamekuwa kwenye ugomvi tangu bebe cool amshauri aachane na matumizi ya dawa za kulevya la sivyo atapotea kimuziki.

King Saha alikasirisha na kauli hiyo ambapo amekuwa akimchana Bebe Cool kwenye mahojiano mbali mbali na hata akaachia disstrack iitwayo Zakayo ambayo inalenga bossi huyo wa Gagamel.

Eddy Kenzo kipindi cha nyuma alikuwa kwenye ugomvi na Bebe Cool lakini baadae wakakuja wakamaliza tofauti zao ambapo kwa sasa wana uhusiano mzuri wa kufanya kazi pamoja.

 

 

 

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke