Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo ana wafuasi wengi ambao wanamwamini katika muziki wake. Mwimbaji huyo amefichua kuwa aliwakatisha tamaa wasanii waliomtaka ajitoze kwenye uongozi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA.
Akizungumza katika mahojiano na runinga moja nchini humo, bosi huyo wa Big Talent ameeleza kuwa wasanii tofauti walimsihi kugombea wadhfa wa urais katika chama hicho kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni lakini alikataa.
Hitmaker huyo wa ngoma “Nsimbudde” anaamini kuwa anaweza kuwatumikia wanamuziki wenzake hata bila kupewa nafasi yoyote katika tasnia ya muziki nchini uganda.
“Nilifuatwa na wanamuziki wengi wakiniomba nigombee urais wa UMA lakini nilikataa, si lazima niwe ofisini ni watumikie, mimi si mwanachama kiherehere wa UMA lakini naunga mkono Chama hicho na kuitakia mema,” alisema. .
Mapema wiki hii, Eddy Kenzo alimuidhinisha Msanii mwenzake King Saha kugombea urais wa cha cha UMA ambacho pia kinang’ang’aniwa na rais wa sasa chama hicho Cindy Sanyu.