You are currently viewing EDDY KENZO AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA BOBI WINE

EDDY KENZO AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA BOBI WINE

Staa wa muziki kutoka Uganda Eddy Kenzo amedai hana uhakika kama uhusiano wake na Bobi Wine utawahi kuwa mzuri tena.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Eddy kenzo amesema licha ya kutozungumza na Bobi wine kwa muda mrefu hana ugomvi wowote na bobi wine huku akisisitiza kwamba ikitokea amempa mwaaliko wa kutumbuiza kwenye onesho lake la muziki atatumbuiza bila kusita.

Utakumbuka mwaka wa 2020 uhusiano kati Bobi Wine na Eddy Kenzo iliingiwa na ukungu mara baada ya sauti ya Eddy Kenzo kusambaa mtandaoni ambapo alisikika akimtolea uvivu bobi wine kwa kumtaja kuwa ni mbinafsi na mnafiki alipodai kuwa alimsaidia kimuziki.

Eddy kenzo kipindi cha nyuma aliwahi fanya kazi na mdogo wa bobi wine, mikie wine chini ya lebo ya muziki ya firebase entertainment ambapo waliachia wimbo wa pamoja uitwao Yanimba ambao ulimfungulia milango Eddy kenzo kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke