Bosi wa Big Talent, Msanii Eddy Kenzo anaonekana kutofurahishwa na kesi dhidi yake kwamba alivunja mkataba alioingia na Luba Events ya kufanya show ya pamoja.
Siku ya Jumatatu, Kenzo aliitwa na polisi wa CPS Kampala kujadiliana na Luba Events juu ya jinsi wanavyoweza kutatua tofauti zao lakini hakujitokeza.
Luba anataka Kenzo amfidie pesa alizowekeza katika kuandaa tamasha la Eddy Kenzo mnamo 2020 kabla ya kufutiliwa mbali kwa sababu ya Covid-19.
Kulingana na mwakilishi kutoka Luba Events, Polisi watatekeleza kwa ufanisi agizo la mahakama linalomzuia Kenzo kutumbuiza jijini Kampala.
Ikumbukwe kwamba Kenzo hivi karibuni alifanya tamasha lake katika Uwanja wa Ndege wa Kololo bila kumhusisha Luba Events.